Ukatili wa kijinsia bado ni kikwazo nchini Tanzania
- 19 Agosti 2016
Tanzania inakabiliwa na kiwango cha
juu cha ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, pamoja na vipigo
kwa wanawake kutoka kwa waume zao licha ya juhudi mbali mbali za kupinga hatua
hiyo na sheria kali kutungwa bado matukio ya aina hii yanazidi kuongezeka.
Utafiti wa hali ya afya ya
uzazi,mtoto na malaria wa mwaka 2015/2016 unaonesha kuwa idadi ya wasichana
wanaopata watoto katika umri wa miaka 15-19 imeongezeka mpaka kufikia asilimia
27 mwaka 2015 kutoka asilimia 23 mwaka 2010.
Kwa muujibu wa utafiti uliofanywa na
UNICEF wa mwaka 2015,Tanzania ina asilimia 3.5 ya watoto wa umri wa miaka 7-17
walio nje ya shule.
Hii inajumuisha watoto takriban
milioni 2 walitakiwa kuwa shule za msingi na watoto takriban milioni 1.5
waliotakiwa kuwa shule za sekondari.
Aidha utafiti huo umetanabahisha
kuwa katika kila watoto watano wa umri wa kuwa shule ya msingi,kuna mtoto
ambaye hayuko shuleni na katika kila watoto watano wa umri wa kuwa shule ya
sekondari kuna watoto zaidi ya wawili ambao hawako shuleni kutokana na sababu
mbali mbali.
Katika harakati za kutokomeza ndoa za utotoni ,ukatili
wa kijinsia kwa mtoto wa kike na wanawake licha ya kuwapa mafunzo maafisa
maendeleo ya jamii ,maafisa ustawi wa jamii na hata polisi na kuwajengea uwezo
wasichana ,vilabu 350 vya wasicha vimeundwa nchini Tanzania ambao wanatambua
haki zao za msingi.
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment