Hakuna fomula au
kanuni maalumu unayoweza
kuitumia kwa kudumu
katika NDOA au
MAHUSIANO YA MAPENZI . Aidha unapokuwa
katika NDOA au
katika mahusiano ya
KIMAPENZI kila siku
inayopita hali huwa
tofauti. Na unachotakiwa KUJIFUNZA
ni kuwa NDOA
au MAHUSIANO YA KIMAPENZI
ni kama MCHE
wa bustanini unaotakiwa KUUPALILIA
na KUUMWAGILIA MAJI
na kuhakikisha haushambuliwi na
WADUDU, MAGUGU , UKAME n.k.
JIULIZE ni
kiasi gani wewe
binafsi umekuwa ukiiangalia NDOA
yako kama bustani
na kiasi gani
umehakikisha kuwa wewe
hujawa chanzo cha
MAGUGU , WADUDU na UKAME
unaokwaza uhusiano wako
wa NDOA na
FURAHA ndani ya
nyumba. Kumbuka ndugu
yagu wewe unaishi
na binadamu. Huishi na
mnyama ambaye hatafakari
kile unachokifanya.
Ni kawaida
ya wanaume wengi
KUJIFIKIRIA wao wenyewe
katika mahusiano yao
ya NDOA. Wakisha maliza
hamu yao ya TENDO LA
NDOA basi hutafuta
shuka na kukoroma
bila kuhakikisha kama
wote mmeridhika au
hapana. NI KWA NDOA
YAKO NA
MAHUSIANO YAKO.
NIKUULIZE
SWALI NDUGU YANGU !
Je, kuna wakati wewe
na mke wako
au mpenzi wako mnafanya MAWASILIANO juu
ya namna ya
kuboresha MAHUSIANO yenu
yaani TENDO LA
NDOA ? NI TENDO LA
MUHIMU SANA
KATIKA KUIMARISHA NDOA. LIJADILIWE LISIACHWE
TAFADHALI !
MAANA
YA MAWASILIANO NI
NINI ? Unapokaa
chini na kumuuliza
mwenzio juu ya
kama ameridhika au
hapana na kuwa
ufanye nini ili
aridhike unaonyesha dalili
ya kuwa UNAMPENDA , UNAMJALI na
kuwa unataka apate
FURAHA ile ile
unayopata wewe. Lakini
hii ni wanaume
wa kiafrika bwana
unakuwa kama---------ndivyo tunvyotukanwa na
wapenzi wetu.
NDUGU yangu usifikiri
VIBAKA wanaokuibia MKE
WAKO wanafuatwa kwa
sababu gani ? -------ni
kwa sababu wanajitahidi kuwaridhisha WANAWAKE
zenu ambao nyie
huwaacha na njaa
kila siku.
Unapofanya mawasiliano uelewe
kuwa unasaidia kutoa
nafasi ya WEWE
KUELEWEKA ZAIDI. Utakuwa
unajipatia FURSA ya
kumweleza MPENZI wako ni
wakati gani hujisikii
kabisa . Na mwenzio atakuelewa .
Usiseme kuwa yeye
si anaona MIMI
nimerudi saa tano
usiku , si anajua nitakuwa
NIMECHOKA . SIO KILA MTU
ANAPOCHELEWA KURUDI KUTOKA
KAZINI ANAKUWA AMECHOKA . MWELEZE KUWA
HUJISIKII NA TOA
SABABU ZA KUELEWEKA. TUZINGATIE SANA
HILI WANANDOA AU WAPENZI.
Kama unaona
kuwa huwezi kwenda
sambamba na mahitaji
ya mpenzi wako
ya mahusiano hayo
basi FANYENI UTARATIBU
WA KUWA NA
RATIBA. Kuwa ijulikane siku
fulani itasaidia na
baada ya wiki
we BWANA au
MKE urudi mapema
au usitafute visingizi. Huenda hii
itasaidia na baada
ya hapo mnaweza
kuanza taratibu kutafuta
namna ya kuongeza
siku na kuboresha
mahusiano yenu.
JE,
NIFANYEJE ILI NDOA
YANGU IDUMU ? Kabla ya KUOA ni
lazima kujua nini
LENGO lako la
kutaka KUOA. Kama UNAOA
bila MALENGO basi
kwako kijana litakuwa
ni TATIZO
KUBWA na MIGOGORO ISIYOISHA. Unapokuwa na
MALENGO kabla ya
KUOA unakuwa umeshatayarisha NYENZO
na MBINU za
namna ya kuyafikia
MALENGO hayo. Kwa
hiyo kama LENGO
mojawapo la KUOA
ni kupata mwenzi
wa kudumu wa maisha
basi ni lazima
utakuwa umetayarisha MBINU
ZA NAMNA ya kufanya
mapenzi yenu yadumu. KAMA
unataka KUOA basi
huna budi kufanya
matayarisho ya kuwa
MUME.
Yaani wewe
ni MWANAUME lakini
inawezekana hujui nini
ukifanye ii jamii
na MKE akuone
kuwa ni mkweli
unafaa kubeba sifa
ya MUME. Kama bado
hujajua inakuwaje basi
unapaswa kwenda shule
na kuhudhuria SEMINA
mbalimbali za NDOA.
ANGALIZO: Unapokuwa MUME
au MKE unapaswa
kuachana na TABIA
ambazo ulikuwa nazo
kabla ya KUOA
au KUOLEWA. Ukiona unakuwa
na majukukmu mgongoni
mwako na unakuwa
na mtu anayekutegemea saa
zote.Naye hakutegemei kwa
chakula tu, anakutegemea kwa
MALAZI, KWA ULINZI WA
MWILI na ROHO
na unakuwa kimbilio
lake kila unapopatwa
na matatizo. UPWEKE ,
UCHUNGU WA ROHO
na kadhalika.
ANGALIZO: KWA WANAUME .Je,
wewe umejitayarisha kuwa
kimbilio la mpenzi
wako katika hali
mbalimbali au wewe
tu ndiye unayetakwa kuwa
mtu anayetunzwa.
Unapokuwa MUME unapaswa
kujua kuwa MKE
wako alipokubali KUOLEWA na
wewe alikuwa na
MALENGO. Ni MALENGO gani
hayo.Tafadhali unapaswa kuchunguza
na kuhakikisha kuwa
MALENGO hayo yanafanana
na yale ya
kwako na kama
hayafanani ni namna
gani unapanga kuyarekebisha ili
muweze kwenda pamoja
katika MTIZAMO. Na kama
ni MALENGO mazuri
hauna budi kuhakikisha kuwa
unamsaidia katika kuyafanikisha.Kama yeye
atafanikisha LENGO zuri
alilojia katika NDOA
basi una uhakika
kuwa MAISHA yenu
yatakuwa hayana matatizo
na UTADUMU NAYE.
MAKALA hii imeandikwa
na MWL. JAPHET
MASATU, anapatikana kwa EMAIL: japhetmasatu@yahoo.com. Call/
WhatsApp + 255 755 400 128 / + 255 716 924 136. Mshirikishe mwenzako. Kama una
swali lolote uliza karibu
tujadiliane tutafute ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment