Wanaume ambao watafanya uasherati kufungwa Cameroon
Wanaume
ambao hushiriki uasherati watafungwa jela, chini ya sheria mpya ambayo
inajadiliwa na bunge la Cameroon.
Mswada
huo ambao ulipata uungwaji mkono wa chama cha Rais Paul Biya, unatarajiwa
kuidhinishwa.
Kwa
sasa wanawake wanaweza kufungwa jela kwa kati ya miezi miwili na sita kwa
kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Wakosoaji
wanasema kuwa sheria hiyo itairudisha nyuma Cameroon, na kusababisha watu wengi
kufungwa.
BBC , SWAHILI , 23/06/2016