Imezoeleka kwamba ndoa za kikatoliki
zikifungwa zimefungwa
pamoja na sharti hilo ,viwango vya ndoa zinazovunjika
zinaendelea kuongezeka na kufuatia hali hiyo,kanisa katoliki limeamua kuanzisha
tuzo maalumu kwa wandoa wakongwe zaidi kwa mwaka huu katika kanisa hilo.
Kanisa Katoliki jimbo kuu la Dar es
salaam wameandaa kliniki ya ndoa ili kuweza kuwapa fursa wanandoa kuimarisha
ndoa zao kiimani,Padre Novatus Mbaula ambaye ni mkurugenzi wa ndoa na familia
anaeleza lengo la kliniki hii ni kuwapa nafasi wanandoa wa katika makundi
mbalimbali kukaa pamoja kupata neno la Mungu na kuweza kuongea juu changamoto
zao mbalimbali kuongea kuhusu maisha yao ya ndoa.
Ni nafasi ambayo wanandoa ambao wana
uzoefu mkubwa katika ndoa wanaweza kuwafaidisha wanandoa wachanga lakini pia
changamoto katika ulimwengu wetu wa sasa changamoto bado ni zilezile.
Pesa
zimeharibu ndoa nyingi
Miongoni mwa watu waliohudhuria
kliniki hii ni wanandoa wenye ndoa yenye miaka 61,brigedia Generali mstaafu
Francis Mbena,mwenye umri a miaka 86 alifunga ndoa akiwa na miaka 25 ,mwaka
1965 Juni,anasema wao zamani walikua wanafuata mtu na familia gani na ina vigezo
gani?
Walikua wanaangalia tabia kama
msichana hana tabia nzuri huoi huko; kama familia ina watu walevi uwaendei na
unatafuta familia yenye watoto wenye tabia nzuri ili na wewe uweze kupata
watoto wenye tabia nzuri.
Wakati mke wake ambaye ni Maura
Stephen Mbena ambaye anasema asili yake ni Nyoni,yeye anasema ukiweza
kumvumilia mwezako na ukamsamehe basi unaishi tu maana kukwaruzana kupo
hakuishi na kikubwa ni kuvumilia.
Na katika mila na desturi za kabila
yake ya wangoni, msichana kabla hajaolewa anaanapewa maneno na wazee ambao
wazazi wako wamewaamini wanakupa msafara wote wa maisha ya ndoa,kwamba
unapokwenda kuna matatizo pengine wakwe zao hawatakupenda au hautafanya vizuri
kule na wanakupa muelekeo wa maisha ukavumilie na ukafanye hivi hivi lakini
kikubwa sana ni sala.
Ndoa ni maisha yenye tafsiri
nyingi,Bwana na bi.Alphonce Hurick walioko kwenye kipindi cha mwaka mmoja wa
ndoa,wao wanaona maisha ya ndoa ni maisha yenye furaha,amani na upendo na ni
maisha tofauti kabisa wakati kila mmoja akiishi peke yake peke yake,kwani hata
kama una msongo wa mawazo kama ndoa yako ina furaha basi hayo matatizo yanakuwa
hayapo kama ndoa yako ina upendo.
Bi.Kigadie ambaye yuko kwenye ndoa
kwa miaka 46 na miezi mitano anaeleza jinsi walivyoingia kwenye ndoa na jinsi
vijana wanavyoingia kwenye ndoa katika miaka ya sasa.
Anasema wengi hawakupata mafunzo ya
kujua uchumba ni nini maana mapema mno wanageuza uchumba kuwa mme na mke kabla
hawajapata sakramenti ya ndoa,sasa hilo ni tatizo ambalo wanajikuta wamepata
ujauzito sasa ndoa inakuwa ya shuruti unaweza kuwa hata bwana alikuwa hana nia
ya ndoa zaidi ya tamaa za kimwili na kimaisha.
CHANZO CHA TAARIFA: BBC SWAHILI, 09/06/2016
No comments:
Post a Comment