Wanaume
na wanawake 50,000 wamesaini azimio la kushinikiza serikali ya India kufutilia
mbali sheria ya kutumia neno Talaq, mara tatu kwa misingi ya kuvunja ndoa.
Kwa
sasa wanaume Waislamu wanaweza kuwataliki wake zao kwa kutamka neno hilo Talaq
mara tatu. Mfumo huo umefutiliwa mbali katika mataifa mengi ya Kiislamu lakini
ungali inakubaliki nchini India.
Kampeini
ya kutaka sheria hiyo ya talaka maarufu talaq kwa kiislamu, kufutiliwa mbali,
imepata uungwaji mkono nchini India.
Maelfu
ya watu wanasaini azimio kuunga mkono kampeini hiyo inayoongozwa na shirika la
kina mama nchini India la BMMA, ambalo limeandikia barua kwa shirika kuu la
kutetea haki za kina mama likitaka sheria hiyo kufutiliwa mbali.
Shirika
hilo limesema kuwa sheria hiyo imeharibu maisha ya kina mama wengi na watoto na
mwaka wa 2015 lilitoa ripoti ambayo ilibainisha zaidi kesi mia moja kuhusiana
na sheria hiyo iliowalishwa.
Azimo
kama hilo pia liliwasilishwa mbele ya mahakama ya juu zaidi nchini humo na mama
mmoja ambaye alitalakiwa na mumewe kupitia barua.
CHANZO CHA HABARI : BBC SWAHILI, 01 JUNI ,2016
No comments:
Post a Comment