Thursday, 23 June 2016

WANAUME AMBAO WATAFANYA UASHERATI KUFUNGWA CAMEROON



Wanaume ambao watafanya uasherati kufungwa Cameroon

 

Wanaume ambao hushiriki uasherati watafungwa jela, chini ya sheria mpya ambayo inajadiliwa na bunge la Cameroon.
Mswada huo ambao ulipata uungwaji mkono wa chama cha Rais Paul Biya, unatarajiwa kuidhinishwa.
Kwa sasa wanawake wanaweza kufungwa jela kwa kati ya miezi miwili na sita kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Wakosoaji wanasema kuwa sheria hiyo itairudisha nyuma Cameroon, na kusababisha watu wengi kufungwa.

BBC , SWAHILI , 23/06/2016