MWANAUME na MWANAMKE
wanaweza tu kuridhishana katika
uhusiano wao kama
kila mmoja atahusika
kikamilifu kufanikisha UHUSIANO
huo , hali kila mhusika
akizingatia kwamba kuna
wakati ambapo kunaweza
kukawa na DOSARI.
Jambo la
msingi katika katika
uhusiano wao ni
HESHIMA. Kila mmoja amheshimu
mwenzake. Kwa kawaida pale
ambapo hapatakuwa na
HESHIMA ina maana
kila mhusika hafahamu
MAHITAJI YA MWENZAKE.
MUME au
MKE , anaweza akawa hafahamu
nini mwenzake anahitaji, matokeo yake, CHUKI
huweza kujitokeza katika
NDOA, hatimaye wanaweza KUTENGANA
kwa sababu ya
HASIRA au sababu
nyingine yoyote.
Sizungumzi kwa
NIA ya kutoa
kipaumbele kwa MAHITAJI
YA TENDO LA
NDOA zaidi, kwani MWANAMKE
na MWANAUME HUOANA
hali kila mmoja
akifahamu bayana kile
kinachoendelea bila kukizungumzia.
Hakika kuelewa
huko hakuwezi kuwepo
wakati wote ,kwani wakati
mwingine mtu hawezi
kuelewa MAHITAJI YA
MWENZAKE hadi aambiwe na
hata akiambiwa hawezi
kuelewa mara moja.
Mke anaweza akawa
na dhana kuwa
kama kweli MUMEWE
anampenda , ni LAZIMA AFAHAMU
MAHITAJI YAKE. MUME anaweza
akawa anampenda sana
mkewe , lakini asijue
kile kinachosababisha AKASIRIKE , AHUZUNIKE au
kuwa na HASIRA. Anaweza tu
kufahamu kuwa uhusiano
wao si mzuri
kwa sababu ya
HASIRA.
Watu wengi
HUOANA bila kuzingatia
umuhimu wa KUHESHIMU
MAWAZO YA WENGINE , mbali ya
kujifunza KUPOKEA na
KUTOA.Kutakiwa kutoa maelezo
haina maana ya
kutokuwepo kwa UPENDO
au maelewano baina
ya WAPENZI , wala isidhaniwe
hivyo.
UHUSIANO MZURI
ni ule ambao
ni zaidi ya
maneno matupu.Mbali ya
MAWASILIANO ya mdomo , ni
lazima wahusika wabadilishane mambo
ambayo si ya
kuzungumza.KILA MMOJA ATOE
MAWAZO YAKE NA
YASIKILIZWE , YAWE YA KIMAPENZI, CHUKI AU
HUZUNI.
WENGINE hudhani kuwa
HISIA ZA CHUKI
humaanisha kuwa UHUSIANO
umeingia DOSARI. Dhana hiyo
si sahihi. Watu wa
namna hiyo huwa
na mawazo ambayo
si sahihi na
kudhani kuwa kama
UNAMPENDA fulani , hamwezi
MKAKASIRIKIANA. Si kweli ndugu
yangu. Ni ishara ya
ukomavu katika mahusiano. KUGOMBANA katika
MAHUSIANO ni jambo la
kawaida USIOGOPE . KAA NA
MWENZAKO NA MUONGEE
ILI KUTATUA MIGOGORO
ILIYOPO KATI YENU.
HISIA ZA HASIRA
huweza kusaidia kupunguza
fukuto la chuki
ambalo huweza kuwa
nalo.Huweza kutokea maudhi
baina ya
watu wowote wenye
UHUSIANO , lakini ni vizuri
kulizungumzia jambo lolote
linalokuudhi kuliko kuliachia
libakie ndani ya
MOYO wa mtu , kisha
lisababishe KUTENGANA.
Hata hivyo, watu
wanaamini kuwa ni lazima watarajie
kuona mambo fulani
yakitokea katika NDOA , ambayo kwa
kawaida hayatokei au hayatokei
mara moja. Hivyo , kutokana na
kupungukiwa UZOEFU , MUME au
MKE huweza kuwa
na WASIWASI juu
ya kuridhishana kwao.
Kuna
WANAUME ambao wanadhani
kuwa lazima kila
wakati wawaridhishe wake
zao , na kwamba , pale wanaposhindwa kuwaridhisha wanafanya
kinyume na WAJIBU
wao. Katika hali halisi , hakuna MTU
anayeweza kumridhisha mwenzake
wakati wowote ule
na kwa namna
yoyote ile kwa
sababu sisi si
MALAIKA. TAMBUA HILO.
NDUGU YANGU
nilianza mapema kuzungumzia
kuwa HESHIMA ndiyo
jambo la MSINGI
katika kufanikisha UHUSIANO
WA MUME NA
MKE.Ina maana kila
mmoja awe tayari
KUMSIKILIZA MWENZAKE na
KUAMINI kuwa kile
ambacho mwenzake anazungumza
NI MUHIMU.
ANGALIZO KWA
MUME NA MKE –Watu hawapaswi
kudhani kuwa kila
jambo litakwenda safi
mara tu baada
ya KUOANA. Michezo ya
kuigiza , picha za filamu
na habari zinazotolewa kwenye
televisheni huweza kuishia
huko , lakini kazi ya
NDOA huanzia huko.
KAZI KUBWA ni
kuzingatia HESHIMA, USHIRIKIANO,
MAWASILIANO na MAELEWANO.
Hayo katika mahitaji
yote ya NDOA
ni muhimu , likiwemo TENDO
LA NOA ambalo
huweza kufikia kiwango
cha kuridhishana zaidi
kadri MUDA unavysonga
mbele , badala ya kuwahi
sana kuruhusu mawazo
ya KUSHINDWA.
WATU hawazaliwi wakiwa
wanafahamu kila jambo
ambalo ni lazima lifahamike .Hawapaswi kutegemea
MAFANIKIO ya mara
moja kwa sababu
yanahitaji MUDA na
KUFANYA KAZI KWA
BIDII.
Asante kwa kusoma
MAKALA hii . Mshirikishe mwenzako. Mungu akubariki.
MWANDISHI wa MAKALA
hii ni MWL.
JAPHET MASATU , anapatikana kwa
EMAIL : japhetmasatu@yahoo.com. Mobile no /
WhatsApp + 255 755 400 128 / + 255 716 924 136. Kwa USHAURI , MAONI Tuwasiliane.